D-Mannose ndicho kiungo kikuu kinachotumika katika Super Eco. D-Mannose ni aina ya sukari inayopatikana katika matunda kadhaa na imethibitishwa kuwa na ufanisi kama wa antibiotiki katika kutibu UTI. D-Mannose huzuia bakteria kushikamana na kuta za kibofu. Zaidi ya hayo, Super Eco ina Vitamini C, ambayo huongeza kinga yako, hutia asidi kwenye mkojo, na kuzuia ukuaji wa bakteria. Super Eco inapatikana katika vidonge vyenye ladha ya chungwa, vinavyoweza kutafunwa. Mchanganyiko wa D-Mannose na Vitamin C unapendekezwa na madaktari na kuungwa mkono na utafiti wa kisayansi kutumika peke yake au pamoja na antibiotiki ili kudhibiti UTI.
Tumia Super Eco kwa afya njema ya mfumo wa njia ya mkojo.
Kunywa vidonge vinne (4) kila siku pamoja na maji au juisi kabla ya milo. Vidonge vya Super Eco pia vinaweza kumung’unywa au kutafunwa. Super Eco inapatikana kwa matumizi ya kila wiki - vidonge 28 na matumizi ya kila mwezi - vidonge 120.
Super Eco inapatikana kwa njia ya mtandao kupitia www.yebihealth.co.tz.
Pia inapatikana kwenye maduka ya dawa / famasi kote nchini.
Imenisaidia sana katika kupunguza UTI ya mara kwa mara. Daktari alipendekeza niitumie kuzuia maambukizi ya UTI. Pia ngozi yangu imeanza kunawiri tangu nianze kutumia Super Eco.
Nina miaka 27 na nimekuwa na UTI tangu nianze kujamiiana. Kwa sasa nina mpenzi mpya na nimekuwa nikiipata mara kwa mara. Baada ya kumaliza dozi ya antibayotiki, nilipata UTI tena baada ya wiki chache na nimekuwa naogopa hata kufanya ngono. Ila tangu nianze kutumia Super Eco, tatizo hili limeisha kabisa. Naomba hali iendelee hivi hivi.
I had frequent urinary tract infections for years. Nothing helped, mpaka nilipoona Super Eco mtandaoni. I took them as per instructions and it was gone within a couple days. Kiukweli zimenisaidia sana.
Nilikuwa nikisumbuliwa na UTI kipindi chote chau ujauzito. Nilipata Super Eco mwishoni mwa ujauzito ikanisaidia sana. Tangu wakati huo na miezi tisa sasa baada ya kujifungua ninatumia Super Eco na sijapata UTI tena.
Nashukuru nimetumia Super Eco kwani imenisaidia sana. Ninaendelea kutumia kama kirutubisho kuzuia nisipate UTI kirahisi tena.
Ndugu yangu alimpa dada aliyepata UTI kali baada ya kujifungua. Huyo dada alipona chap bila kutumia dawa nyingine.
Nilikuwa nasumbuliwa na UTI ya muda mrefu. Pia nilikuwa napata mkojo wa njano wenye harufu kali
Mwanzoni sikuwa na imani ila baada ya kuitumia kwa siku tatu nikawa sisikii maumivu. Baada ya wiki nikaenda kupima na kuambiwa sina UTI.
Nimependa kirutubisho hiki na ninakipendekeza kwa yeyote mwenye UTI. Nilikuwa na UTI sugu ila dawa hii imefanya kazi ya kushangaza. Mimi hutumia vidonge 3 mara mbili kwa siku ninapohisi dalili au baada ya kujamiiana. Kisha huchukua vidonge 2 asubuhi na 2 usiku, wakati mwingine 2 asubuhi na 2 usiku kulingana na ninavyohisi.
Mimi hupata UTI mara kwa mara kwa hiyo daktari wangu aliniambia nijaribu Super Eco. Huwa napata maambukizi ya UTI kutokana complication za dawa nyingine ambazo huwa nitumia. Baada ya kuanza kutumia Super Eco pamoja na hizo dawa, nimekuwa vizuri kwa muda mrefu sana. Huwa natumia vidonge viwili asubuhi na viwili jioni kama ilivyoandikwa kwenye kikopo cha dawa.
Baba yangu ana umri wa miaka 70 na amekuwa na catheter kwa miaka mitatu sasa. Kabla ya kutumia Super Eco, baba alikuwa akiugua UTI mara kwa mara. Miezi minne sasa tangu aanze kutumia Super Eco hajapata UTI.
Mimi hutumia kidonge kimoja kila siku kwa ajili ya kuzuia kupata UTI. Iwapo nahisi dalili yoyote ya UTI hata kidogo huwa nameza vidonge 2 mara mbili kwa siku. Huu mpango umenisaidia sana na sasa sisumbuliwi na UTI.
Aisee, dawa zenu nimezipigia saluti. Leo nimeenda hospitalini kupima UTI na kukutwa sina baada ya kutumia Super Eco kwa siku tatu tu.
Je, kiungo kikuu kwenye Super Eco ni nini?
Kiungo kinachofanya kazi kwenye Super Eco ni D-Mannose. D-Mannose ni aina ya sukari inayopatikana katika matunda na mboga mboga kadhaa ambayo inaaminika kuzuia kunasa kwa bakteria kwenye seli za kibofu cha mkojo. Haimeng’enywi katika miili yetu kama sukari zingine na kwa hivyo haitegemewi kuwa na athari kwa viwango vya sukari ya damu. Hata hivyo ikiwa una kisukari inashauriwa umjulishe daktari wako na kufuatilia kiwango chako cha sukari kwenye damu mara kwa mara ili kuwa salama. Pia Super Eco ina Vitamin C inayoongeza kinga mwilini na kung’arisha ngozi.
D-Mannose inafanyaje kazi?
D-Mannose huzuia uwezo wa bakteria kushikamana na seli za kibofu. Hivyo bakteria hawawezi kushikamana na kuta za kibofu kwahio hutolewa nje kwa mkojo.
Je, kuna ushahidi kwamba Super Eco inafanya kazi?
Ndio, tafiti za kisayansi zimeonyesha ufanisi wa D-Mannose dhidi ya UTI ya kawaida na UTI sugu inayojirudia.
Je, nahitaji kutumia Super Eco hata kama sina UTI?
Ndio, Super Eco ni kirutubisho kinachozuia UTI ya mara kwa mara au kutibu UTI hai. Dozi zinazopendekezwa kutibu UTI hai ni gramu 1.5 mara mbili kwa siku kwa siku 3, na kisha mara moja kwa siku kwa siku 10; au gramu 1 mara tatu kwa siku kwa siku 14. Kuzuia UTI mara kwa mara tumia gramu 2 mara moja kwa siku, au gramu 1 mara mbili kwa siku kwa wiki 2 hadi 6.
Naweza kutumia Super Eco pamoja na dawa au virutubisho vingine?
Hakuna utafiti unaonyesha jinsi D-Mannose inavyoweza kuingiliana na dawa nyingine na virutubisho vingine. Zungumza na daktari ikiwa una wasiwasi.
Naweza kutumia Super Eco nikiwa mjamzito au wakati nanyonyesha?
D-Mannose huvumiliwa vizuri na watoto na watu wazima. Hakuna tafiti zilizoangalia kama D-Mannose ni salama wakati wa ujauzito au kunyonyesha.
Je, kuna madhara yanayoweza kutokana kwa kutumia virutubisho hivi?
Watu wachache wanaweza tumbo kujaa gesi au kupata choo laini.
Naweza kutumia Super Eco nikiwa na kisukari?
Ikiwa una ugonjwa wa kisukari, zungumza na daktari wako kabla ya kutumia D-Mannose. Daktari wako anaweza kufuatilia viwango vya sukari yako ya damu kwa karibu zaidi ikiwa unatumia D-Mannose.
Wanaume wanaweza kutumia Super Eco?
Ndio, wanaume pia wanatumia Super Eco. Japo kuwa tafiti nyingi zimefanywa kwa wanawake. Wanaume waliotumia Super Eco wamekuwa wakipata matokeo mazuri.
Je, ninaweza kumeza kidonge cha Super Eco?
Kama ilivyo kwa dawa zote, fuata maagizo kwenye maelezo ya bidhaa kuhusu jinsi ya kutumia Super Eco.
Ninapaswa kutumia Super Eco kwa muda gani?
Dozi zinazopendekezwa kutibu UTI hai ni gramu 1.5 mara mbili kwa siku kwa siku 3, na kisha mara moja kwa siku kwa siku 10; au gramu 1 mara tatu kwa siku kwa siku 14. Kuzuia UTI mara kwa mara tumia gramu 2 mara moja kwa siku, au gramu 1 mara mbili kwa siku kwa wiki 2 hadi 6.
Nini kitatokea nikiacha kutumia Super Eco?
D-Mannose imeonesha kufaa kwa matibabu ya muda mrefu ya kuzuia UTI inayojirudia na inaweza kuchelewesha kujirudia kwa UTI baada ya matibabu, lakini maambukizo yanaweza kujirudia baada ya kuacha kuitumia kwa muda mrefu.
Itachukua muda gani mpaka nianze kupata matokeo?
Hii inaweza kutofautiana kulingana na aina ya UTI lakini kwa ujumla mabadiliko huonekana ndani ya masaa 48. Hata hivyo, ikiwa una homa au huna nafuu basi ni muhimu kumuona daktari kwa matibabu zaidi.
Je, Super Eco ni salama kwa watoto? Kuanzia umri gani?
D-Mannose ni sukari na kwa ujumla huvumiliwa vizuri kwa watu wazima na watoto. Dozi itahitaji kubadilishwa kulingana na umri wa mtoto. Wasiliana na daktari wa mtoto wako kabla ya kutumia D-Mannose.
Je, napaswa kunywa maji kwa kiasi gani wakati wa kutumia Super Eco?
Tumia kila dozi na glasi ya maji na hakikisha unakunywa maji ya kutosha kwa mahitaji ya mwili.
Je, manufaa yatabaki kwa muda gani baada ya kuacha kutumia Super Eco?
Hili lipo tofauti kwa watu tofauti. Ni vyema kutumia mara kwa mara kwa kinga hasa kama umekua ukipata UTI za mara kwa mara. Pia Super Eco ina Vitamin C ambayo husaidia kuimarisha kinga ya mwili. Hivyo inashauriwa kutumia mara kwa mara.
Je Super Eco imethibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS)?
Ndio, kirutubisho hiki hii kimesajiliwa na kuthibitishwa na Mamlaka ya Viwango Tanzania (TBS).
info@yebihealth.co.tz au tembelea duka letu la mtandaoni: https://yebihealth.co.tz
Copyright © Yebi Health. All Rights Reserved.